MTANGAZAJI

MSIBA BOTSWANA

Jana saa 2.30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki blog hii ilipata taarifa za msiba wa mke wa Dr Mgeni (wa pili kutoka kulia waliosimama) imeelezwa kwamba kifo cha mama huyo kimesababishwa na ajali mbaya baada ya gari dogo alilokuwa amepanda Marehemu akiwa na mama mwingine walipokuwa wakielekea kazini asubuhi jana huko Botswana alikokuwa akiishi kugongana uso kwa uso na lori

Pichani juu ni wakati kundi la waimbaji wa Royal Advent Quartet toka Morogoro,Tanzania lilipofanya ziara nchini Swaziland mwaka 2002 ambako familia ya Dr Mgeni ilikuwa ikiishi kabla ya kuhamia kikazi nchini Botswana. Mwili wa Marehemu unatarajiwa kusafirishwa kuja Tanzania kwa mazishi.

BLOG HII INATOA POLE KWA FAMILIA YA DR MGENI,NDUGU JAMAA NA MARAFIKI POPOTE WALIPO

2 comments

mumyhery said...

Poleni kwa msiba Mwenyeezi Mungu awape moyo wa subira

Mzee wa Changamoto said...

POLENI Ndugu, jamaa na marafiki. Na Mungu ailaze mahala pema roho ya Dr Mgeni

Mtazamo News . Powered by Blogger.