MTANGAZAJI

KIRUMBA ADVENTIST CHOIR-2006


Baadhi ya waimbaji wa KIRUMBA ADVENTIST CHOIR(MWANZA)

Kama kunakwaya ambayo naiheshimu hapa nchini Tanzania ni Kirumba Adventist Choir ya mjini Mwanza nakumbuka nilianza kuimba pale mwaka 1990, nikitokea Mabatini hukohuko jijini Mwanza,na nilipofika hapa nilipata changamoto kubwa kutokana na uimbaji wa nyimbo za nota kwani nilikuwa sijawahi kuimba aina hii ya umbaji na nakumbuka aliyenisaidia sana wakati huo kunipa msingi wa uimbaji ni marehemu Richard Maira aliyetoka kwaya ya Magomeni SDA na kuhamia Mwanza.Nakumbuka wimbo ulionisumbua sana ni ule wa "Kuna nchi nzuri sana" na ule wa sauti za kiume(Male voice)"Pendo la Mungu" uliomo katika mojawapo ya albamu mpya za kwaya hii inayotarajiwa kutoka hivi karibuni.
Niliimba katika kwaya hii hadi mwaka 1995 nilipohamia Morogoro,Tanzania

Kwaya ya Kirumba ambayo ina albamu zisizopungua sita za audio na mbili za video kukua kwake hadi kufikia hapo ilipo kumechangiwa sana na Mwalimu wake wa muda mrefu Mzee Josia Sagatti(wa kwanza kulia mwenye suti ya kijivu) ambaye ni Baba mzazi wa Ahadi Sagatti ambaye ni mwimbaji wa kundi la Magomeni Heralds,The Peace,mmoja wa viongozi wa
A cappella Kwanza Tanzania na Mkurugenzi wa Sagatti Graphics Limited.

Waimbaji kama vile James Gayo(Kingo),Tony Onditi,Godfrey Jonathan,Ahadi Sagatti,Hulda Malegesi,Jack Ndugu n,k ni matunda ya kwaya hii na wamechangia kwa kiasi kikubwa kuifikisha ilipo sasa

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.