A CAPPELLA KWANZA TANZANIA
Kikundi cha waimbaji wa A cappella kinachojulikana kwa jina la Sonda ya Dilu toka Ukonga,Dar es Salaam
Baadhi ya viongozi wa A CAPPELLA KWANZA TANZANIA,Kutoka kushoto ni Maduhu(Katibu),Amani(Mwenyekiti),Enosi(Mratibu/Mawasiliano) na Yusuph(Makamu Mwenyekiti)
A cappella Kwanza ni kikundi cha kijamii chenye makao makuu yake jijini Dar es salaam,kinachojihusisha na shughuli za sanaa ya muziki wa A cappella.Ni kikundi kilicho na lengo la kusimamia,kukuza na kuendeleza fani ya muziki wa A cappella ikiwa kama sehemu mojawapo ya kuhubiri neno la Mungu na kutoa elimu kwa jamii juu ya uwepo wa utajiri wa kihistoria wa sanaa ya muziki wa A cappella.Ninapozungumzia A cappella ninamaanisha uimbaji usiotumia ala za muziki.
Msingi wa A cappella ni wa kihistoria ulianza karne nyingi zilizopita,Ulianza ambapo jamii za makabila mbalimbali zilikuwa zikiimba nyimbo za kidini,muziki huu pia ulianza zamani kabla ya hata ya ugunduzi wa vyombo vya muziki.
Mpaka sasa hakuna taasis ama kikundi chochote ambacho kimekuwa kikijihusisha na maendeleo ya muziki wa A cappella nchini Tanzania mbali na kikundi cha A CAPPELLA KWANZA kilichosajiliwa mwaka 2006 na Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA),Morning Star radio na AWR-Morogoro.
Hapa Tanzania aina hii ya uimbaji imekuwa ikitumiwa sana na kwaya ama vikundi vya makanisa mbalimbali kama vile,Kanisa la waadventsita,kanisa la kiinjili la kirutheri,kanisa la baptist n.k
Vikundi ambavyo vimekuwa vikiimba muziki wa A cappela ni The Voice,Tukumbukeghe Singers,Royal Advent Quartet,Ilala Male Chorus,Busy Bee Quartet,Magomeni Trio,Zanzibar Brothers,Magomeni Heralds,Sonda ya Dilu Singers n.k
Kwa mara ya kwanza hapa nchini A CAPPELLA KWANZA itafanya kongamano la uimbaji wa A cappella katika ukumbi wa Msimbazi Center jijini Dar es salaam March 11,2007 ambapo Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki,Mhe.Hulda Kibacha atakuwa mgeni rasmi
Kwa maelezo zaidi kuhusu kongamano hilo tembelea:
Post a Comment