MTANGAZAJI

NITAPITA ULIPOPITA


Mchungaji Michael Kuyenga ndani ya Morning Star FM


Natumaini u mzima na ninafurahi tena kukutana nawe kukufahamisha yale yanayojili hapa AWR-Morogoro,Tanzania.

Aliyekuwa mtayarishaji na mtangazaji wa matangazo ya Redio ya Waadventista Uliwenguni , idhaa ya kiswahili Mchungaji Lusekelo Mwakalindile amejiunga na kituo cha redio kinachomilikiwa na Kanisa la Waadventista nchini Tanzania,Morning Star 105.3 FM kilichopo Mikocheni B,jijini Dar es salaam.

Lusekelo ambaye alikuwa kipenzi cha wasikilizaji lukuki kutokana na kutangaza kipindi cha SIRI ZA USHINDI kutokana na kugusa maisha halisi ya wasikilizaki katika suala zima la kufanikiwa katika maisha kiroho,kijamii, kielimu na kiuchumi anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa kituo cha Morning Star,Mchungaji Michael Kuyenga ambaye kwa sasa ni Afisa Uhusiano wa Chuo Kikuu cha Arusha cha Kanisa la Waadventista,Tanzania kilichoko Ngongongare,Usa River,Arusha.

Kinachotia changamoto ni kwamba wakati Mchungaji Lusekelo anachukua nafasi ya kuwa mwandaaji wa vipindi vya AWR hapa Morogoro miaka mitano iliyopita Mchungaji Michael Kuyenga ndiye aliyemwachia jukumu hilo wakati huo akielekea nchini Uingereza kuchukua masomo ya Mawasiliano ya Umma na ndiye sasa tena amemwachia jukumu lingine la kutumika pale Morning Star,hakika "NITAPITA ULIPOPITA NA KUACHA ALAMA ZA NYAYO ZAKO"

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.