MTANGAZAJI

HOPE CHANNEL INTERNATIONAL YAZINDUA STUDIO ZA MAUDHUI YA FILAMU

 


Hope Channel International (HCI) imezindua idara mpya ya Uinjilisti, Hope Studios, inayolenga kutayarisha maudhui ya filamu kwa majukwaa mbalimbali, kwa lengo la kufanya  uinjilisti.
Derek Morris, Rais wa HCI, na Vyacheslav Demyan, makamu wa rais wa HCI anayesimamia vipindi, walisisitiza kwamba mpango huu unalenga kufikia hadhira ya kimataifa, kuvuka mipaka ya kijiografia na tofauti za kitamaduni.
Hope Studios inapanga kuunda anuwai ya maudhui yenye athari, ikiwa ni pamoja na filamu za simulizi na hali halisi.
Studios hutumikia katika majukumu mengi kwa upande wa maudhui  ndani ya mtandao wa HCI, ikiwa ni pamoja na kuunda maudhui mapya, kutenda kama kiunganishi cha studio za nje, na kujadili leseni za usambazaji wa maudhui ya  watu wengine.
Kuanzishwa kwa Hope Studios kulitangazwa katika Kongamano la Uongozi la Mtandao wa Hope Channel huko Johannesburg, Afrika Kusini, mwezi wa Aprili 2023,Ambapo Waliohudhuria walieleza kufurahishwa na kujitolea upya kwa utengenezaji wa filamu.
Kwa namna inavyoendelea mbele katika tasnia ya vyombo vya habari vya Kanisa, HCI inahimiza kuhusika katika mpango huu.Inaalika watazamaji kufuatilia filamu katika HopeStudios.org, kuzishiriki na wengine, na kuunga mkono misheni ya HCI kupitia maombi na michango ya kifedha.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.