MTANGAZAJI

VIONGOZI WA MAKUNDI YA WHATSAPP KUFUTA UJUMBE


 

Mtandao wa kijamii wa WhatsApp uko katika majaribio ya kuwaongezea nguvu viongozi wa makundi ya mtandao huo kuwa na uwezo wa udhibiti ikiwemo kufuta ujumbe wa watumiaji wa makundi hayo.

Mtandaoni huo unafanyia majaribio kipengele kipya kinachojulikana kama “admin detele” kwa baadhi ya watumiaji wa simu zenye mfumo endeshi wa Android.

Kipengele kipya cha Admin delete kitawaruhusu wasimamizi wa kikundi kufuta ujumbe wowote wa washiriki katika kikundi chao.

Hiyo huenda aikasaidia kuongeza nidhamu katika makundi hayo na kuzuia maudhui yasienda na malengo ya kuanzishwa kwa kundi husika. Hata hivyo, kipengele hicho kisipotumika vizuri kinaweza kuvunja haki za watumiaji wa mtandao huo ikiwemo uhuru wa kujieleza na kutoa maoni.

Admin akifuta ujumbe wa kikundi utatoweka kwa kila mtu, na kuacha taarifa kwamba umefutwa na msimamizi.

Kipengele kingine kipya kizuri kinachofanyiwa kazi ni Chatbot, ambacho kitawanufaisha watumiaji wa matangazo ndani ya programu hiyo. 

Matangazo hayo yatajumuisha arifa (notification) kuhusu vipengele vipya vya WhatsApp, vidokezo na mbinu, na ikiwezekana ujumbe kuhusu ofa zinazolipishwa. 

Kumbuka pia mapema mwaka huu, WhatsApp ilianza kujaribu kipengele kingine ili kuboresha matumizi ya mtumiaji, kuwezesha uwezo wa kuhariri ujumbe wako.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.