BALOZI KOMBO AKUTANA NA WADAU WA NGO JIJINI ROMA
Balozi wa Tanzania nchini Italia Mahmoud Thabit Kombo amekutana na kufanya mkutano na wadau wa Taasisi zisizo za kiserikali (NGO) takribani sitini na nne zinazofanya shughuli zake nchini Tanzania mwishoni mwa juma Jijini Roma, Italia.
Mkutano
huo ulihudhuriwa pia na wadau mbalimbali wa Diaspora pamoja na wadau wa
NGO walimpongeza Balozi kwa kuwapa nafasi ya kujitambulisha na
kutoa fursa ya kuwasikiliza mafanikio yao sambamba na changamoto
wanazopitia katika kufanikisha shughulika zao nchini Tanzania.
Pamoja
na kuwasikiliza lakini pia Balozi alitumia nafasi hiyo kuwashauri kuwa
na ushirikiano wa pamoja ili kuleta ufanisi zaidi kwenye maeneo wanayo
yafanyia kazi. Aidha, katika mkutano huo Balozi Kombo aliongea mubashara
na Balozi wa Italia nchini Tanzania Mhe. Marco Lombardi na kumpa fursa
ya kutoa salaam zake moja kwa moja kwa njia ya mtandao.
Balozi
wa Italia nchini Tanzania aliwahakikishia wadau hao kuwa wapo kwenye
mikono salama ya Balozi wa Tanzania Rome na chini ya uongozi wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan kuwa
Tanzania ni nchi salama ya kufanya shughuli zao.
Post a Comment