MTANGAZAJI

POLISI AUAWA WAKATI AKITAFUTA NYUMBA

 Afisa wa polisi wa Los Angeles ambaye hakuwa kazini amepigwa risasi na kuuawa katika tukio la  wizi alipokuwa akitafuta nyumba na mpenzi wake, maafisa wamesema.
 
 Idara ya Polisi ya Los Angeles imemtambua Polisi huyo kuwa ni Fernando Arroyos (27) ambaye alishatumikia jeshi hilo  kwa miaka mitatu katika Kitengo cha Olimpiki.
 
 Tukio hilo lilitokea Jumatatu jioni katika jengo la  1700 katika mtaa wa 87 Mashariki huko Los Angeles, imeeleza  Idara ya Polisi ya Kaunti ya Los Angeles, ambayo inaongoza uchunguzi.
 
 Mkuu wa Polisi Michel Moore aliwaambia wajumbe wa Bodi ya Makamishna wa Polisi Jumanne kwamba Arroyos aliuawa katika ufyatulianaji wa risasi na wanaume watatu waliojaribu kumwibia.
 
 Arroyos alikuwa akitafuta nyumba ya kununua na mpenzi wake ndipo walipofuatwa na wanyang'anyi, ambao wawili kati yao walifyatua risasi, wapelelezi wamesema.
 
 Arroyos alimwambia mpenzi wake kukimbia na yeye kurushiana risasi na watu hao lakini alipigwa, Moore aliwaambia wajumbe wa bodi kwamba Arroyos alikuwa na matarajio ya maisha mazuri ambayo "yamechukuliwa" katika wizi wa barabarani.
 
 Wanaume watatu na wanawake wawili ambao majina yao hajatajwa wanashikiliwa na Polisi,hakuna wamezuiliwa, hakuna hata mmoja ambaye ameshtakiwa kwa mauaji, Taarifa ya  ya Polisi imesema. 
 
 
 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.