WAZIRI GWAJIMA KUZIKABILI NGOs KOROFI TANZANIA
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,
Wazee na Watoto wa Tanzania Dkt. Dorothy Gwajima amesema Serikali haitavulia kuona
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanafanya kazi nchini humo bila kufuata sheria.
Dkt. Gwajima amesema hayo Bungeni Jjijini Dodoma
wakati kuwasilisha Hotuba ya Mwelekeo wa Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa
mwaka wa fedha 2021/2022.
Amesema Serikali itaendelea kuimarisha ufuatiliaji na uratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali ili yatoe mchango Chanya wa Ujenzi wa Taifa na hivyo kunufaisha Jamii.
Amesema pamoja na jitihada zinazoendelea kufuatilia na kuratibu shughuli za Mashirika hayo, Serikali itahakikisha jitihada zaidi inaongeza kukomesha Mashirika yasiyotimiza masharti.
" Sitokubali kuona Shirika lolote lisilo la Kiserikali kuona linafanya kazi bila kusajiliwa kwa mujibu wa Sheria sitovumilia hili litokee jisajilini mfanye kazi kwa utaratibu” alisema Waziri Gwajima.
Amesema shilingi milioni 585.5 zimetengwa kwa aliji ufuatiliaji wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali 1,000 Tanzania Bara.
Waziri Gwajima pia amezungumzia umuhimu wa kukuza Uzalendo wananchi na ari ya kujitolea kujiletea Maendeleo yao kwa kutumia rasrimali zinazowazunguka ambapo ushungi milioni 350.7 zimetengwa kufanikisha azma hiyo.

Post a Comment