MTANGAZAJI

WAZIRI AHIMIZA MOTISHA KWA WATUMISHI TANZANIA

 

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Tanzania, Mwanaidi Ali Khamis amemuagiza Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt John Jingu kutumia Wataalam wake kusimamia majukumu ya Wizara kuhakikisha watumishi wanafanya kazi kwa weledi.

 

Naibu Waziri Mwanaidi ametoa agizo hilo jijini Dodoma wakati akifungua Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Afya-Idara ya Maendeleo ya Jamii liliofanyika katika ukumbi wa Makao ya Taifa ya Watoto ya Kikombo.

 

Amesema kuwa Wizara inatakiwa kuwatumia ipasavyo watumishi wake katika kuhakikisha mipango iliyowekwa inasimamiwa na kutekelezwa kikamilifu ili kuboresha huduma za Wizara hiyo na kutatua changamoto mbalimbali katika jamii.

 

 Aidha, amewataka watendaji katika ngazi mbalimbali kuweka mkakati mbalimbali wa kutatuzi wa changamoto za jamii ikiwemo tatizo la ndoa za katika umri mdogo na vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia.

 

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya-Idara ya Maendeleo ya Jamii Dkt John Jingu amesema lengo la Baraza hilo la Wafanyakazi ni kushirikiana watumishi katika mipango na utekelezaji wa majukumu ya Wizara.

 

Dkt. Jingu amesisitza kuwa vikao  vya Baraza la wafanyakazi ni kiunganishi muhimu kinachoweza kuiwezesha Menejimenti na Watumishi kufanya kazi kwa weledi na kuondokana na dukuduku miongoni mwa wafanyakazi.

 

Ameongeza kuwa Baraza la Wafanyakazi likifanikiwa kufanya kazi zake vizuri, wafanyakazi watatimiza wajibu wao kwa kuzingatia maadili na weledi wa hali ya Juu.

 


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.