MTANGAZAJI

KAMPUNI YA KOREA YAKABIDHI VIFAA VYA UCHUNGUZI WA CODIV 19 KWA SERIKALI YA ZANZIBAR

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman akikabidhiwa Vifaa vya Maabara vya uchunguzi wa Covid 19, vilivotolewa na Kampuni ya SD Biosensor ya Korea akikabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vital Supplies Limited ya Tanzania Bw. Jimmy C Apson. hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar, na (kushoto kwa Makamu) Waziri wa Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee,Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui na (kulia kwa Mkurugenzi) CEO wa Vital Supplies Limited Bw.Sanjay Patadia wakipika makofi wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano.


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa Vifaa vya Maabara kwa ajili ya Wizara ya Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee,Jinsia na Watoto Zanzibar, vilivyotolewa na Kampuni ya SD Biosensor ya Korea, kwa ajili ya uchunguzi wa Covid 19, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.

Waziri wa Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee,Jinsia na Watoto Zanzibar. Mhe Nassor Ahmed Mazrui, akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa Vifaa vya Maabara vya uchunguzi wa Covid 19.

Makamu  wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman akiwa na viongozi wa serikali wakiwemo  Viongozi wa Wizara ya Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee,Jinsia na Watoto Zanzibar wameshiriki hafla ya kukabidhiwa Vifaa vya Maabara vya Vipimo vya Uchunguzi wa Covid 19, vilivyotolewana Kampuni ya SD.Biosensor ya Korea  katika viwanja vya ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar  Mei 21,2021..

 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.