MTANGAZAJI

DKT CARLTON BYRD AWA MWENYEKITI WA KONFERENSI YA WAADVENTISTA

 
Dkt. Carlton P. Byrd ambaye ni Mhubiri maarufu katika Kanisa la Waadventista wa Sabato na
aliye hubiri kwa mkutano Injili wa MUNGU Kwanza uliofanyika Chato,Tanzania Februari 2020 amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Konferensi ya Kusini Magharibi ya Kanisa la Waadventista wa Sabato nchini Marekani,uchaguzi huo unafuatia Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Konferensi hiyo kilichoketi hivi karibuni jijini Dallas,Texas.
 
Taarifa ya kuchaguliwa kwa  Dkt Byrd zimetolewa katika Ukurasa Rasmi wa Konferensi ya Kusini Magharibi kwenye mtandao wa Facebook.

Konferensi hiyo ni inayojumuisha eneo la majimbo ya Texas,Louisiana na Arkansas ni miongoni mwa Konferensi tano zinazounda Unioni ya Kusini Magharibi ambako wakazi wake wengi ni Wamarekani Weusi ambapo kuna wakazi wapatao 3,957,986  huku takwimu za Juni 2008 zikionesha kuwa Unioni hiyo ilikuwa na makanisa 100 yenye waumini 23,020  ikimiliki shule 9 na walimu 18.
 
Dkt. Carlton P. Byrd ambaye alihubiri kwa mkutano Injili uliofanyika Chato,Tanzania Februari 2020 ulioandaliwa na Kanisa la Waadventista wa Sabato na Umoja wa Wajasiriamali na Wanataaluma Waadventista Tanzania (ATAPE) na kurushwa na vyombo vya Habari vya Kanisa hilo alikuwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Oakwood linalohudumia watu 2,800  na Mkurugenzi wa Kituo cha Breath Of Life kilichoko Alabama, Marekani .

 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.