WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUZINGATIA WELEDI
Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania Dkt.
Hassan Abbasi amewataka Waandishi wa Habari nchini humo kutekeleza majukumu
yao kwa weledi ili kuepuka makosa ya kisheria yanayoweza kujitokeza.
Dkt.
Abbasi ameyasema hayo leo jijini Dodoma alipokuwa akitoa mada juu ya
''Matumizi ya Mitandao ya Kijamii''' wakati wa mafunzo kwa Waandishi wa
Habari za mtandaoni wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)
(TBConline).
Amewataka kutojiona wanyonge kwa
kufanya kazi hiyo, bali wajione watu waliobeba dhamana kubwa katika
kuihabarisha jamii mambo mbalimbali yanayoendelea duniani.
"Si
lazima Waandishi wote wa Habari waonekane kwenye Televisheni, kuna
namna nyingi za kufanya kazi hii ikiwemo mitandao ya kijamii ambayo
watumiaji wake wanaongezeka kwa kasi, kwa sasa dunia imehama kutoka
mtaani kwenda mtandaoni." amefafanua Dkt. Abbasi.
Post a Comment