WAADVENTISTA TANZANIA KUANZISHA GAZETI
Taasisi ya Vyombo vya Habari vya Kanisa la Waadventista wa Sabato Tanzania (TAMC) inatarajia kuanzisha Gazeti liitwalo Sauti Kuu, kuanzia Januari 23 mwaka huu.
TAMC inayomilikiwa na Kanisa la Waadventista wa Sabato nchini Tanzania ndiyo ambayo inasimamia Morning Star Radio na Kituo cha Televisheni cha Hope Channel Tanzania vilivyopo jijini Dar es salaam,Rock FM ya jijini Mbeya na Studio za Redio ya Waadventista Ulimwenguni (AWR) zilizoko Morogoro.
Taarifa toka TAMC zinaeleza kuwa Uzinduzi wa Gazeti hilo ambalo litakuwa likitoka mara moja kwa juma likiwa na habari mbalimbali za kijamii,kiroho,burudani na makala za Afya na Familia.unatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es salaam,
Post a Comment