MTANGAZAJI

MUUZA MADAWA YA KULEVYA ALIYETAKA KUTOROKA JELA AKUTWA AMEKUFA (+VIDEO)


Muuza Madawa ya Kulevya raia wa Brazil Clauvino da Silva (42) ambaye alijaribu kutoroka kwa kuvaa nguo za binti yake na kisha akagundulika,amekutwa amekufa gerezani Agosti 6,2019,taarifa zinaeleza kuwa Clauvino aliyekuwa akitumikia kifungo cha miaka 73 kwa kujihusisha na madawa ya kulevya inaonekana alijiua.

Agosti 4,mwaka huu Da Silva alijaribu kutoroka gerezani  akijitambulisha kuwa ni binti yake mwenye miaka 19 akiwa amevalia nguo za kike na sura bandia akitaraji kuwa atatoroka katika gereza hilo lenye ulinzi mkali ambapo,askari  walimgundua na kumrekodi video wakati akivua mavazi ya kike aliyokuwa amevaa.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.