MTANGAZAJI

WATANZANIA UINGEREZA WACHAGUA VIONGOZI WA JUMUIYA - ATUK

 
Hatimaye Watanzania Uingereza tumewachagua viongozi wa Jumuiya yetu ( Association of Tanzanians UK) yaani ATUK. Juni 2018 mkutano mkuu ulifanyika mjini Reading kufukuzia zoezi hili chini ya ulezi wa Balozi Mheshimiwa Asha Rose Migiro. Mchecheto ulifukuzwa na wengi ila aliyewasha kiberiti alikuwa Joseph Warioba. Baada ya mwaka, siku nzima ya Mtanzania, Jumapili 30 Juni , 2019, ilitayarishwa na wanakamati wa ATUK – ambao baadhi walikuja kuwa viongozi wa Jumuiya. Hapa inaonyesha namna juhudi za Balozi kutuunganisha zilivyoambatanika na ari na hamasa za Watanzania.
Azma kuu ya Jumuiya hii si tu kukutanisha Watanzania kama sauti moja. Pia kuweka ngazi ya kusaidia , kujenga na kuwekeza nyumbani kutokea huku Majuu. Ni jambo la kuchangamkiwa sana. Watanzania toka sehemu mbalimbali za Uingereza walijieleza na kutafuta kura wakipigania nafasi za uenyekiti, katibu na mweka hazina na makaimu wao. Nusu ya kampeni hizi iliendelea mtndao wa WhatsApp na nusu ikakamilika ofisi za ubalozi wetu mtaa wa Bond Street, London, Jumapili 14 Julai, 2019. Uongozi mpya wa ATUK. Waliosimama nyuma. Toka kushoto, Mweka Hazina Msaidizi, Nelson Kampa, (Birmingham); Naibu Katibu, Frank Leo (Coventry), Mweka Hazina, Lucy Shigikile (London). Walioketi, toka kushoto,: Makamu Mwenyekiti, Zuhura Mkwawa (Leicester), Mwenyekiti , Martha Mpangile (London) na Katibu wake, Dk Imani Kondo... Mwanahabari mkongwe na Mhariri wa The East African, Deo Kamuhanda, akiwa na Simon Mzuwanda (aliyepigania kijasiri wadhifa wa Uenyekiti na kushindwa ), Patricia Mpangala na Joe Wairoba, aliyefanya kazi kubwa kuisimamisha, ATUK.

Alex Masuguri mmmoja wa wasimamizi wakuu wa shughuli hii muhimu akitangaza matokeo. Wenzake ni kushoto, Batilda Tenga na kulia, Pauline Nzengula.
Mwenyekiti mpya, Martha Mpangile, ( pili kutoka kushoto) na Mweka Hazina , Lucy Shigikile (wa kwanza kulia ) wakipongezwa na kina mama wenzao.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.