TCRA YAAGIZA KUWEPO KWA HUDUMA BORA ZA MAWASILIANO KWENYE UJENZI MRADI WA UMEME MTO RUFIJI
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeagiza kuwepo kwa
huduma bora za Mawasiliano katika eneo la Mradi wa ujenzi wa bwawa la kufua
umeme wa maji Mto Rufiji Mkoani Pwani.

Akizungumza wakati wa ziara ya Wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA, kwenye eneo la Mradi huo hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu
wa TCRA Mhandisi James M. Kilaba alisema, Mradi huo mkubwa ni mradi wa kimkakati
na TCRA kama msimamizi wa sekta ya Mawasiliano hapa nchini inaamini hakuna
uwekezaji unaotendeka bila ya uwepo wa mawasiliano, jamii na watu watakaokuwa
wanatekeleza ujenzi wa mradi huo wanapaswa kuwa na mawasiliano ya uhakika wakati
wote wakiendelea na kazi ya ujenzi.
Ujenzi wa Mradi huo wenye thamani ya Shilingi za Kitanzania
Trilioni 6.5 fedha za Serikali, ulizinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli juzi Ijumaa Julai 26, 2019 na
utakamilika mwaka 2022 ambapo utakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme Megawati 2115.
Akieleza zaidi Mhandisi Kilaba alisema, Shirika la TTCL kama
Shirika la Serikali pamoja na watoa huduma wengine ya mawasiliano wanaowajibu wa
kuhakikisha mawasiliano yapo na TCRA wajibu wake ni kuhakikisha watoa huduma wanafanya yale
wanayopaswa kufanywa.
“Hapa umesema zaidi ya wafanyakazi 6,000 watakuwa kwenye eneo
hili, lakini pia hata watakaokuwa wanakuja kufanya utalii kwenye National Park
ya Nyerere ni lazima wawe na mawasiliano na mawasiliano ya sasa ni Data,
kwahiyo tunachoweza kuagiza hususan TTCL ni kuhakikisha wanaenda kwa kasi kubwa
kuweka mawasiliano katika eneo hili na mawasiliano tunayotaka sisi kama
wadhibiti ni 4G as Minimum.” Alifafanua Mhandisi Kilaba na kuongeza
“Kwa hiyo 4G siyo isubiri mpaka turbines (mitambo ya kufua
umeme)zianze kuzunguka, la hasha, ujumbe tunaowapa kwakweli mwisho wa mwezi wa
Nane (Agosti) mwaka huu, watu waanze kupata huduma za 4G katika maeneo haya.”
Alisisitiza.
Hata hivyo alielezwa tatizo la mawasiliano ya simu linalokabili eneo la mradi na kuomba TCRA kuyahimiza makampuni ya simu kuboresha huduma zao.
.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jones Killimbe (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi James M. Kilaba (wapili kushoto) na mmoja wa wajumbe wa bodi, wakiwa kwenye eneo la Mto Rufiji ambako kunajengwa bwawa la kufua umeme wa maji Megawati 2115.
Baadhi ya wajumbe wa bodi na menejiment ya TCRA wakiwa kandokando ya Mto Rufiji Julai 28, 2019 wakati wa ziara ya kutembeela ujenzi wa Mradi wa umeme wa Mto Rufiji. |
Msafara wa TCRA ukipatiwa maelezo ya utekelezaji wa Mradi.
Post a Comment