HIFADHI YA TAIFA YA BURIGI-CHATO KUFUGULIWA JULAI 9,2019
Waziri
wa Maliasili na Utalii,Dkt Hamis Kigwangallah akizingumza wakati
akifungua Mkutano Mkuu baina ya Shirika la Hifadhi za Taifa
(TANAPA),Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari Waandamizi ,Mkutano
unaofanyika katika ukumbi wa mikutano katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa
Mwanza.
Waziri
wa Malisili na Utalii ,Dkt Hamisi Kigwangallah amesema Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anatarajia kufungua
rasmi Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato siku ya Jumanne ya Julai 9,2019 .
Dkt
Kigwangallah ametoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka
baina ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ,Wahariri na Waandishi wa
Habari Waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya Habari nchini ,mkutano
unaofanyika jijini Mwanza.
Amesema Serikali inakamilisha mkakati wa kuanzisha utalii wa Majini katika
maeneo ya Hifadhi na Vivutio vilivyopo ndani na Pembezoni mwa Ziwa
Victoria "Boti Maalumu kwa ajili ya kusafirisha watalii kati ya maeneo
ya Hifadhi zilizopo katika ukanda huu inatarajia kufika Mwanza hivi
karibuni "alisema Dkt Kiwangallah .
Akimkaribisha
Dkt Kigwangallah ,Kamishna wa Uhifadhi (TANAPA) Dkt Allan Kijazi
amesema mkutano huo unafanyika kwa miaka sita mfululizo ni mkakati wa
kuwawezesha wana habari kufahamu na kuelewa masuala ya Uhifadhi ili
waripoti kwa usahihi mambo mblimbali yanayohusua Uhifadhi na Utalii kwa
ujumla.
Post a Comment