MTANGAZAJI

ULIVYOKUWA UZINDUZI WA FIELD YA KATI MWA TANZANIA YA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO (+VIDEO)


Kuzinduliwa kwa Field Mpya ya Kati mwa Tanzania katika Kanisa la Waadventista wa Sabato (CTF) kulikorushwa mbashara kupitia HopeChannel Tanzania na Morning Star Radio  kumefanyika Dodoma nchini Tanzania ambapo ulifanywa na Dkt Blasious Ruguri ambaye ni Kiongozi wa Kanisa hilo katika Kanda ya Afrika Mashariki na Kati (ECD) Machi Mosi mwaka huu.
 Uzinduzi huo pia ulishuhudiwa na Viongozi wa Kanisa hilo katika kanda ya Afrika Mashariki na Kati,Unioni ya Kusini mwa Tanzania na Unioni Konferensi  ya Kaskazini mwa Tanzania.
  Waliochaguliwa kuongoza CTF ambayo itajumuisha mkoa wa Iringa,Dodoma na sehemu ya wilaya ya Kiteto ni
Mch Toto Bwire Kusaga-Mwenyekiti
Mch Festo Mng'ong'o-Katibu
Joshua Mwambopo-Mhazini
Wakurugenzi ni
Mch David Mmbaga-Idara ya Shule Sabato na Huduma Binafsi
Mch Yared Nkoswe-Idara ya Uwakili
Mch Sabato Maseke-Idara ya Huduma za Vijana 
Mch Harold Lissi-Idara ya Uchapishaji
Janeth Bwaira-Idara ya Huduma za Wanawake
Field hiyo itakuwa na wajumbe 16 wa Kamati ya Utendaji.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.