MCHUNGAJI GEOFFREY MBWANA ANAENDESHA MKUTANO WA INJILI HUKO ELDORET NCHINI KENYA
Mkutano wa Mkubwa wa Injili wenye kauli mbiu ya Kuikimbilia Medali ya Matumaini umeanza huko Eldoret nchini Kenya,ambao unahudumiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Ulimwenguni Mch Geoffrey Mbwana toka nchini Marekani,Mch Njuguna toka Kenya na Hesperance Deodate toka Tanzania ambaye ni mtalaamu wa masuala ya lishe kwa binadamu.
Katika Mkutano huo wa majuma mawili unaendeshwa kwa lugha ya kiswahili Mchungaji Njuguna anatoa mafundisho ya Kaya na Famili na Hesperance Deodate akitoa mafundisho ya afya na Mchungaji Geoffrey Mbwana akifundisha neno la Mungu ambapo amekuwa akitumia vielelezo vya maisha halisi ya wanariadha wa nchi ya Kenya wanaotoka Eldoret walioshinda medali mbalimbali za mashindano ya riadha duniani akiwemo Felix Kirui ambaye alishinda medali huko China mwaka 2015.
Waimbaji wa kwaya ya Nyegezi toka Mwanza na Gospel Flames toka Tanzania ni miongoni mwa waimbaji wanaohudumu kwenye mkutano huo ambao unarushwa Mbashara na Hope Channel Kenya na Hope Channel Tanzania kila siku saa 10:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki
Post a Comment