MTANGAZAJI

VIONGOZI WA MATAWI YA TAUS NCHINI MAREKANI WAPATIWA MAFUNZO NA KIONGOZI WA KANISA ULIMWENGUNI


Makamu wa Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Ulimwenguni Mchungaji Geofrey Gabriel Mbwana kwenye mkutano huo.

Viongoni wa Matawi ya Umoja wa Watanzania Waadventista nchini Marekani (TAUS) yaliyoko katika majimbo mbalimbali nchini humo walikuta huko Maryland kwa ajili ya kupatiwa mafunzo ya Uongozi,mafunzo ambayo yalitolewa na Makamu wa Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Ulimwenguni Mchungaji Geofrey Gabriel Mbwana.

Mafunzo hayo ambayo alikuwa ya kwanza toka Kongamano la Mwaka lililofanyika julai mwaka huu huko Winscosin yalijikita katika masuala ya Umoja,Uongozi na Upangaji wa Mikakati yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo viongozi hao ambao miongoni mwao walichaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka huu katika nyadhifa  mbalimbali za uongozi wa TAUS.

TAUS toka ilipoanzishwa huko Marekani  mwaka 1999 ikiwa na wanachama wapatao 300 kwa sasa,imekuwa ikijihudisha na mikakati ya uwezeshaji wa miradi mbambali ya Elimu,Uinjilisti na Afya nchini Tanzania ikiwemo ujenzi wa Makanisa,Kusaidia Wainjilisti,kusomesha wachungaji n.k.

Waweza kupata maelezo zaidi kuhusu TAUS kwa kutembelea katika tovuti yao ambayo ni www.tausinc.org

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.