MTANGAZAJI

WAIMBAJI WAWILI WA THE LIGHT BEARERS KUFUNGA NDOA OKTOBA 22,2017 JIJINI DAR ES SALAAMWakati waimbaji wa The Light Bearers toka Tanzania wakirejea nchini leo baada ya kuwepo nchini Marekani kwa muda wa siku 45,moja wapo ya mambo yanayosubiriwa kwa sasa kutoka kwa waimbaji hao ni ndoa ya waimbaji wawili wa The Light Bearers ambao ni wachumba.

Gisaba toka Sengerema,Mwanza mwimbaji,fundi mitambo,mpiga kinanda na Mhitimu wa shahada ya kwanza ya sheria toka Chuo Kikuu cha Dar es salaam atafunga ndoa na Jacque Solomon mwimbaji wa sauti ya kwanza.

Fuatilia video  maalum iliyotengenezwa na Tegemea Champanda aliyeko Uingereza kuhusu huduma ya waimbaji hawa wawili ambao watafunga ndoa Jumapili ya Oktoba 22,mwaka huu saa sita mchana katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato Mbweni jijini Dar es salaam


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.