UZINDUZI WA MAISHA HATIMAYE 2018 WAFANYIKA MBEYA
Mkutano wa Maisha Hatimaye unaotarajiwa kufanyika jijini Mbeya mwezi Februari mwaka 2018 ukiratibiwa na Chama cha Wajasiriamali na Wanataaluma Waadventista nchini Tanzania (ATAPE) umezinduliwa rasmi hivi karibuni huko Mbeya na Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania Mchungaji Mark Walwa Malekana.
Mkutano wa Maisha Hatimaye utarushwa na Mbashara na Morning Star Radio na Morning Star Televisheni toka Mbeya na kuonekana ama kusikika katika nchi mbalimbali duniani,huku Mnenaji akiwa ni Makamu wa Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Ulimwenguni Mchungaji Geofrey Gabriel Mbwana toka nchini Marekani.
Post a Comment