WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI WA REMNANT GENERATION WAIBUKA NA TUZO TATU ZA UIMBAJI MAREKANI
Waimbaji wa nyimbo za Injili wa kundi la Remnant Generation toka Kanisa la Waadventista Wa Sabato Mwenge jijini Dar es salaam Tanzania wamepata tuzo tatu kwenye tamasha la uimbaji la Diaspora Talents lililofanyika hivi karibuni huko Winston Kaskazini mwa Carolina nchini Marekani ambako walishiriki.
Mama Anna Matinde kiongozi wa kundi hilo amesema leo kuwa Mwimbaji wa Kundi hilo Edna Matinde ambaye ni binti yake alipewa tuzo ya Diaspora Gospel Talent katika kipengele cha Mwimbaji wa kujitegemea.
Kwenye tamasha hilo kuwalikuwa na waimbaji toka Tanzania,Nigeria,Marekani na Uingereza
Wakiwa nchini humo pia walipata nafasi ya kuimba katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato la Winston Salem.
Post a Comment