MTANGAZAJI

TAUS YACHANGIA MILIONI 27 KWA AJILI YA MIRADI YA UTUME TANZANIA


 Image may contain: 21 people, people smiling, crowd, tree, child, sky, grass, shoes, outdoor and nature

Mkutano wa Umoja wa  Watanzania Waadventista waishio Marekani  (TAUS)umemalizika hivi karibuni ambapo watanzania hao wakichangia Dola za Kimarekani 12,000 sawa na Shilingii 27 Milioni za Tanzania kwa ajili ya miradi ya utume wa Injili nchini Tanzania.

Mkutano huo uliohudhuriwa na Makamu wa Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Duniani Mchungaji Geofrey Gabriel Mbwana ,Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Vijana ya Kanisa hilo duniani Mchungaji Pako Edson Mokgwane,Mchungaji David Mmbaga toka  Dodoma,Tanzania ulifanyika Columbus,Wisconsin  ambapo hotuba za neno la MUNGU na mada mbalimbali za ujasiriamali,usimamizi wa Biashara  na uendelezaji wa miradi mbalimbali nchini Tanzania 

Wajumbe wa mkutano huo toka katika majimbo mbalimbali nchini Marekani wengine wakiwa na familia zao waliungana kwa pamoja katika kuchangia fedha hizo ambazo zitakwenda kusaidia kwa awamu kuendeleza  miradi ya kuwasomesha wachungaji,ujenzi wa makanisa na vyombo vya habari.

TAUS ilianzishwa mwaka 1999 huko Massachusetts na wanachama 25 kwa lengo la kuwatanisha Waadventista Watanzania walioko nchini humo ambapo kwa sasa inawachama wapatao 300.Waweza kutembelea katika tovuti yao ambayo ni www.tausinc.org 






No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.