MTANGAZAJI

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AELEZA UJIO WA WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA NCHINI TANZANIA KESHO MACHI 31, 2017


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akisikiliza na kujibu maswali ya waandishi wa habari mapema leo katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa Mjini Dodoma
Baadhi ya Wakurugenzi wa Manispaa za Jiji La Dar es salaam wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul  Makonda wakati akizungumza na Waandishi wa habari
Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda wakati akielezea ujio wa Waziri Mkuu wa Ethiopia 
(Picha Zote Na Mathias Canal-Dodoma)



Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe Hailemariam Desalegn anataraji kuwasili nchini Tanzaniza kesho Machi 31, 2017 katika uwanja wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ziara ya Siku tatu kwa kuitikia Mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ambaye ndiye atakuwa mwenyeji wake.

Taarifa ya ujio wa Waziri huyo Mkuu wa Ethiopia imetolewa hii leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda wakati akizungumza na waandishi wa habari  katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa Mjini Dodoma.

Makonda ameeleza kuwa Mhe Desalegn anataraji kuwasili nchini saa tatu kamili asubuhi Machi 31, 2017 hadi April 1, 2017 ambapo atakuwa nchini kwa shughuli mbalimbali za kidiplomasia zinazogusa nyanja muhimu za kiuchumi, Biashara, na Ushirikiano baina ya Nchi ya Ethiopia na Tanzania.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.