MTANGAZAJI

DAR ES SALAAM:TUME KUCHUNGUZA KUUNGUA KWA CHUMBA CHA MIZIGO UWANJA WA NDEGE JIJINI DAR ES SALAAM


 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu hatua zilizofikiwa na serikali baada ya kutokea moto huo. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Gabriel Migile na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Profesa Ninatubu Lema.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea. 

 Paa la chumba kilichoungua.
 Waandishi wa habari wakiangalia chumba hicho.
 Chumba namba mbili cha kutunzia mizigo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), kikiwa kimetekea kwa moto uliotokea jana usiku katika uwanja huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.


Serikali ya Tanzania  imeunda tume ya watu 12 kwa ajili ya kuchunguza tukio la kuungua moto chumba namba mbili cha kuhifadhia mizigo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) uliotokea jana.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa alisema tume hiyo itaongozwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Joseph Nyahende na itafanya kazi ya uchunguzi kwa muda wa mwezi mmoja kisha kutoa taarifa kamili cha chanzo cha moto huo

Akizungumzia kuhusu tukio hilo alisema moto huo ulitokea jana usiku kwenye chumba namba mbili cha kuhifadhia mizigo ya abiria katika uwanja huo hata hivyo thamani ya vitu vilivyoungua bado haijajulikana.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.