MTANGAZAJI

DAR ES SALAAM:SERIKALI KUANZISHA TUZO KWA WAANDISHI WA HABARI WA MITANDO YA KIJAMII


Serikali ya Tanzania  inatarajia kuanzisha tuzo za umahiri kwa waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii (blogs) nchini kuanzia mwaka 2017.

Katika hotuba yake ya kufunga Mkutano Mkuu na semina ya wanachama wa umoja wa waendeshaji wa blog nchini jijini Dar es salaam leo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (Pichani)amesema kuwa lengo la tuzo hizo ni kuzisaidia blogs za Tanzania kubobea katika nyanja tofauti ikiwemo kilimo, mifugo, viwanda, hifadhi ya jamii kwa nia ya kuipa heshima tasnia ya habari nchini.

Waziri Nape alisema kuwa tayari Serikali imeanza mazungumzo na   makampuni na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kudhamini tuzo hizo ili kuhakikisha kuwa washindi wanapatikana kwa uwazi.
Waziri Nape pia amewataka wamiliki na watendaji wa blogs nchini kushirikiana na Serikali ili kuweza kuijenga nchi.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.