MTANGAZAJI

WAADVENTISTA WA SABATO WATAKIWA KUPINGA RUSHWA

Waumini wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato nchini Tanzania wametakiwa kujiepusha na vitendo vya Rushwa.

Agizo hilo limetolewa na Afisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) wilaya ya Mpwawa Bi Nerry Mwakyusa wakati wa sherehe za uzinduzi wa kanisa la Mlimali zilizohudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa taasisi za Serikali,Magereza na Kanisa la Waadventista Wa Sabato.

Bi. Nerry Mwakyusa aliwaambia waumini wa kanisa la Waadventista Wa Sabato na Watanzania kwa ujumla kuwa rushwa ni adui mkubwa wa maendeleo hivyo waumini wanapaswa kuwa mstari wa mbele kupambana na huyo adui kwa kutoshiriki vitendo vya rushwa na kuwa majasiri kuwafichua wale wote wanaoshiriki vitendo vya rushwa.

Bi. Mwakyusa amesema pamoja na kuwa Rushwa ni kosa la Jinai kwa mujibu wa sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007 lakini pia kwa wakristo rushwa ni dhambi kwa mwenyezi Mungu kwa mujibu wa maandiko matakatifu  Biblia.

Aidha Bi. Mwakyusa ametoa wito kwa waumini wa kanisa jipya la Mlimani pamoja na wahubiri wa injili kuikemea dhambi ya rushwa wazi wazi kwa kuwa rushwa ni kinyume na sheria za nchi na kanuni za kiimani.

Kwa upande mwingine, akitoa salamu za Mkuu wa Gereza Mpwapwa afisa Magereza Joseph Sabayo aliwaeleza waumini wa kanisa la Waadventista Wa Sabato kuwa wengi huchukulia Magereza kama sehemu ambapo watu hufanyiwa ukatili na mateso jambo ambao si kweli. 

Magereza ni sehemu ya urekebishaji wa tabia za watu na mahali pa kujifunza.
Bwana Sabayo amesema, wapo watu walifika gerezani wakiwa hawajui kusoma na kuandika wakatoka gerezani wakiwa wanajua kusoma na kuandika na wapo waliotoka gerezani wakiwa na elimu ya kilimo na wengine hata shahada za sheria na ujuzi mwingine.

Kanisa jipya la Mlunga liko kilometa 76 kutoka Mpwapwa mjini na lina washiriki wapatao 26 na shughuli zao za kiuchumi ni kilimo pamoja na ufugaji.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.