WAPENZI WA NYIMBO WASABABISHA THE LIGHT BEARERS WASHINDWE KUREKODI VIDEO YAO JIJINI LONDON JANA
Mtayarishaji wa Video Tegemea Champanda akiwa na Waziri Barnabas Kiongozi wa The Light Bearers |
Waimbaji wa The Light Bearers jana walisafiri kwa muda usiopungua saa moja hivi toka Mji wa Reading wanakoshiriki mkutano wa Injili na kuelekea jijini London ikiwa ni katika zoezi la kutengeneza video yao wakiwa nchini humo kwa muda wa majuma matatu.
Mtayarishaji wa Video na Miongoni mwa waratibu wa ziara ya waimbaji hao toka Tanzania,Tegemea Champanda anayeishi nchini humo ameiambia tovuti hii kuwa waimbaji hao wamekuwa gumzo na jana ilikuwa waanze shooting lakini shughuli ilikuwa pevu maana kila walipokuwa wakianza kuimba watu walikuwa wanajaa kusikiliza na kusababisha waache kurekodi jambo ambalo pia liliwavuta polisi kuwepo katika eneo hilo na kusikiliza nyimbo za waimbaji hao.
Post a Comment