MTANGAZAJI

OSHA KUJA NA MBINU MPYA ZA KUWASAIDIA WAFANYAKAZI

 Wakala wa Afya na Usalama sehemu za Kazi nchini Tanzania (OSHA) wameeleza kuwa wataboresha ukaguzi wao hasa kwa wafanyakazi walio na UKIMWI jinsi wanavyohudumiwa na waajiri wawapo kazini.

Kaimu meneja usajili na takwimu za afya na Usalama OSHA, Dk. Abdalssalaam Omary ameeleza kwa wanahabari kuwa  kupitia mafunzo waliyoyafanya hivi karibuni wanataraji kuboresha ukaguzi zao ambazo zifanywa katika maeneo ya kazi ambazo zinakuwa zinawahusu watu walio na UKIMWI.

Anasema pamoja na kujipanga kuboresha kaguzi zao alisema kuwa bado wamekuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo kwa muda mwingine zinaweza kuwa zinawafanya wakwame na kueleza changamoto hizo ni pamoja na fedha na madaktari kwa ajili ya kuwafanyia uchunguzi wafanyakazi.

Kwa upande wa serikali kupitia Kaimu Kamishna wa Kazi Msaidizi, Rehema Moyo anaeleza kwa kuna sheria ambazo zimewekwa ambazo zinakataza waajiri kufanya vitendo vya ubaguzi kwa wafanyakazi na hivyo kama kuna waajiri wanawafanyia vitendo ambavyo havikubaliki kisheria basi watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakani kujibu mashitaka yanayowakabili.


Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza mwendeshaji wa mafunzo hayo, Andrew Christian ambaye yupo Geneva, Switzerland aliyekuwa akitoa elimu kuhusu ukaguzi kwa wafanyakazi.



Mwendeshaji wa mafunzo, Andrew Christian akiwa Geneva, Switzerland ambaye alikuwa akitoa elimu kuhusu ukaguzi kwa wafanyakazi.
Wafanyakazi wakiwa katika picha ya pamoja.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.