MTANGAZAJI

TANZANIA YAFANIKIWA KUHUSIKA KATIKA MRADI WA MAFUTA GHAFI

Aprili 23 ,2016 Tanzania imefanikiwa kupata Bomba la mafuta ghafi baada ya Mhe Yoweli Museveni Rais wa Jamhuri ya Uganda kutoa kauli ya mwisho kuwa Mradi wa  Bomba la Mafuta ghafi utapita Njia ya  Kaskazini mwa Tanzania hadi Bandari ya Tanga. 

Kauli hiyo imetolewa saa 7 mchana Aprili 23 katika mkutano wa 13 wa Northern Corirodor uliofanyika Munyonyo Nje Kidogo ya Jiji la Kampala. Kauli hiyo ilitolewa mbele ya marais wa Kenya, Rwanda, na Wawakilishi wa Sudan Kusini, Ethiopia, Tanzania, DRC na Burundi.

Pichani ni timu toka Tanzania wakipongezana na Professor Sospeter Mhongo Waziri anayesimamia Wizara ya Nishati na Madini ambaye alikuwa kwenye msafara toka Tanzania.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.