MAELFU WASHUHUDIA AMBASSADORS OF CHRIST YA RWANDA IKIZINDUA SANTURI MWONEKANO MPYA
Mwalimu wa Ambassadors of Christ Sozzy Joram (Wa Tatu toka Kushoto) akiwaongoza waimbaji kuimba kwenye jukwaa |
Zaidi ya watu 3000 walihudhuria kwenye uzinduzi wa toleo jipya la 12 la Waimbaji wa Ambassadors of Christ liliitwalo Hejuru Mu Kirere (Juu Mawinguni) linalozungumzia nguvu ya MUNGU,tukio hilo la Uzinduzi lilifanyika katika uwanja wa Gitondo mjini Kigali ikiwa pia ni maandalizi ya kwaya hiyo kutimiza miaka 20 toka kuanzishwa kwake,sherehe ambazo zitafanyika mwaka 2016.
Uzinduzi huo uliofanyika Disemba 26 mwaka huu ulihudhuriwa na wapenzi wa nyimbo za Injili toka Tanzania,Kenya,Burundi, Uganda, Zambia na Canada wakiwemo mawaziri wa watatu wa serikali ya Rwanda
Post a Comment