DAR ES SALAAM:HAKI ELIMU KATIKA UZINDUZI WA RIPOTI YA ELIMU KWA MIAKA 10 YA SERIKALI YA AWAMU YA NNE NCHINI TANZANIA
Prof. Martha Qorro (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, John Kalage (kushoto) wakizinduwa ripoti ya Utafiti uliofanywa kuangalia hali ya utekelezaji wa ahadi na utoaji wa elimu hapa nchini katika kipindi cha miaka 10 ya serikali ya Awamu ya Nne iliyoongozwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam |
Prof. Martha Qorro (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, John Kalage (wa pili kushoto) wakionesha nakala za ripoti ya Utafiti uliofanywa kuangalia hali ya utekelezaji wa ahadi na utoaji wa elimu hapa nchini katika kipindi cha miaka 10 ya serikali ya Awamu ya Nne iliyoongozwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete |
Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, John Kalage akizungumza katika uzinduzi wa ripoti ya Utafiti uliofanywa kuangalia hali ya utekelezaji wa ahadi na utoaji wa elimu hapa nchini Tanzania katika kipindi cha miaka 10 ya serikali ya Awamu ya Nne iliyoongozwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete |
Akizungumza
katika hafla ya uzinduzi wa utafiti huo, Mkurugenzi Mtendaji wa
HakiElimu, John Kalage alisema ripoti iliyozinduliwa imeandaliwa na
taasisi hiyo kwa ushirikiano na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM), Profesa Kitila Mkumbo, ambapo kwa ujumla imeangalia ubora wa
elimu ya Msingi na ile ya Sekondari.
Alisema
pamoja na mambo mengine ripoti iliyozinduliwa inaainisha changamoto
zinazoikabili sekta hiyo na namna ya kukabiliana nazo. Alisema matokeo
ya utafiti huo yanaonesha kuwa Serikali ya awamu ya nne imefanya vizuri
katika kupanua fursa za elimu kwa watoto wengi wa Kitanzania, bado
kiwango cha elimu kimeshuka kuliko wakati mwingine wowote katika
historia ya Tanzania ikiwa huru.
"HakiElimu
imekuwa na utamaduni wa kufanya tafiti zenye lengo la kutathmini,
kuainisha na kuibua hari na changamoto za elimu nchini. Tumekuwa
tukifanya tafiti za kila mwaka na tatifi za kipindi fulani kama hii.
Lengo kuu ni kutuwezesha kuwa na taarifa hai juu ya maendeleo ya sekta
ya elimu ili hata tunapoishauri serikali juu ya maeneo ambayo inapaswa
kuboresha au maeneo ambayo imefanya vizuri, tuwe na ushaidi wa kutosha."
alisema Kalage.
Akifafanua zaidi Kalage
alisema kwa upande wa fursa za elimu katika kipindi cha miaka 10 ya JK
kumekuwa na upanuzi mkubwa wa vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo,
ongezeko la idadi ya walimu, vitabu, udahili pamoja na kuhimarika kwa
uwiano wa wasichana na wavulana wanaohitimu elimu ya msingi na
sekondari.
"...Mathalani shule za msingi
zimeongezeka kutoka 14,257 mwaka 2005 hadi 16,538 mwaka 2015 huku
wanafunzi shule za msingi wakiongezeka kutoka 7,541,208 hadi 8,202,892
shule za sekondari kutoka 1,745 mwaka 2005 hadi 4,753 mwaka 2015 huku
idadi ya wanafunzi shule za sekondari wakiongezeka kutoka 524,325 mwaka
2005 hadi 1,804,056 mwaka 2015..." alisema Mkurugenzi Mtendaji huyo wa
HakiElimu.
Aidha alisema katika kipindi hicho
cha JK pia bajeti ya sekta ya elimu ilikuwa kubwa kuliko sekta nyingine
yoyote ikiongezeka kutoka bilioni 669.5 mwaka 2005/2006 hadi shilingi
trilioni 3.4 mwaka 2014/2015, upanuzi huo umewezesha asilimia 98 ya
watoto wanaostahili kupata elimu ya msingi kujiandikisha. Kiwango cha
udahili kwa shule za msingi pia kiliongezeka kwa zaidi ya asilimia 26
kwa ujumla, huku kiwango hicho kikiwa kikubwa zaidi kwa sekondari na
elimu ya juu.
Kwa upande wake Mhadhiri wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Kitila Mkumbo akiifafanua ripoti
hiyo alisema katika mambo ambayo Rais Kikwete alifanikiwa ni kupanua
kiwango cha elimu ya Sekondari na vyuo vikuu jambo ambalo alisema endapo
Rais Dk. John Pombe Magufuli akifuata vyayo zake Tanzania inaweza
kufanya vizuri zaidi kielimu.
Alisema licha ya
uwepo wa changamoto katika sekta hiyo suala la kuwekeza kwa walimu bora
haliepukiki endapo Serikali itaamua kuboresha elimu nchini.
Post a Comment