MWANZA:UNDP YASISITIZA VITA YA UMASKINI KWA KUTUMIA MAZINGIRA
Mkurugenzi
Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Tanzania,
(Ushauri na Miradi), Amon Manyama akitoa maelezo kuhusu mradi wa PEI na
salamu kutoka UNDP kwa washiriki wa mafunzo hayo hivi karibuni jijini
Mwanza.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Amon
Manyama, amesema vita dhidi ya umaskini inakuwa na maana kubwa kama
inalinganishwa na mazingira.
Amesema
kwamba umaskini wa kipato ambao umekuwa ukipiganwa sana kwa sasa
unastahili kupiganwa kwa kuangalia umaskini kutokana na ukweli kuwa
kuboreshwa kwa mazingira ndio hatua kubwa ya kupigana na umaskini katika
sura zote zilizobaki.
Mkurugenzi
msaidizi huyo amesema hayo hivi karibuni mjini Mwanza wakati akielezea
mradi wa mtaji na elimu wa UNDP ambao umefanyiwa kazi kwa pamoja kati ya
shirika hilo, Tume ya Mipango, Hazina na Ofisi ya Makamu wa Rais,
katika mafunzo ya siku moja ya Uimarishaji wa Ushirika wa Akiba na
Mikopo, yaliyofanyika Mwanza.
Mradi
huo umelenga kuwezesha ushirika wa akiba na mikopo katika wilaya sita
nchini kuwezesha wananchi kushiriki katika kukabili umaskini
unaosababishwa na mazingira.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi
Kida akitoa maelezo ya utangulizi juu ya madhumuni ya mafunzo hayo kwa
washiriki kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua rasmi.
Pichani ni baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Ushirika (SACCOS na
VICOBA) na Maafisa Ushirika wa kutoka Wilaya za Bunda, Bukoba na
Sengerema wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa
zikiwasilishwa.
Post a Comment