MTANGAZAJI

MBEYA:MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU AELEZA TAASISI HIYO ILIVYOPAMBANA NA RUSHWA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 10 ILIYOPITA


Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru nchini, Dkt. Edward Hoseah akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa jengo la ofisi mpya ya TAKUKURU Mkoa wa Mbeya ambapo amesema kuwa Taasisi  hiyo imeweza kufanikiwa  kupambana na rushwa  ambapo jumla  kesi kubwa za rushwa 1,993 kuanzia mwaka 2004-2015 zimeweza kufunguliwa ambazo ni sawa na ongezeko la asilimia 81 ikilinganishwa na kesi 384 zilizokuwepo miaka 10 ilioyopita (1995-2004)  .
 
 Amesema ,ongezeko hilo la kesi kubwa limetokana na jitihada za Taasisi hiyo katika kupambana na kuzuia rushwa nchini hasa katika kipindi cha serikali ya awamu ya nne, chini ya rais Jakaya Kikwete.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akitoa salama za mkoa wa mbeya katika hafla ya uzinduzi wa jengo la Takukuru Mkoa wa Mbeya .

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mbeya xavery Mhyella akatoa taarifa ya Takukuru Mkoa wa Mbeya mbele ya Mgeni rasmi katika hafla hiyo ambayo imehudhuriwa na  Mkurugenzi wa Mkuu  Takukuru  nchini Dkt, Edward Hosea Octobar 5 mwaka huu..Picha na Emanuel Madafa ,Jamiimojablog Mbeya 

Mkaguzi Mkuu wa Kanda Takukuru Ndugu Joice Shundi akizungumza katika hafla hiyo.


Wanafunzi wa shule ya sekondari Wende wakitoa burudani za ngoma za asili katika uzinduzi huo wa jengo la ofisi mpya ya Takukuru Mkoa wa Mbeya .




Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa dini waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi wa jengo zilizopo eneo la forest ya zamani karibu na Mahakama kuu jijini Mbeya.






Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru nchini, Dkt. Edward Hoseah akizindua rasmi jengo la ofisi mpya ya TAKUKURU Mkoa wa Mbeya Octoba 5 mwaka huu na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali na taasisi binafsi mkoani humo amabapo jengo hilo limetumia kiasi cha shilingi bilioni 1.2 hadi kukamilika kwakwe.

Muonekano wa jengo la ofisi Mpya za TAKUKURU Mkoa wa Mbeya zilizopo foresti ya zamani karibu na Mahakama kuu jijini humo

Viongozi wa kimila waliohudhuria sherehe hizo.


Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru nchini, Dkt. Edward Hoseah  akipanda mti katika sherehe za uzinduzi wa jengo la ofisi mpya ya TAKUKURU Mkoa wa Mbeya.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akishiriki zoezi la upandaji mti
 katika sherehe za uzinduzi wa jengo la ofisi mpya ya TAKUKURU Mkoa wa Mbeya.




Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru nchini, Dkt. Edward Hoseah akisimikwa kuwa chifu wa kabila la wasafwa katika sherehe za uzinduzi wa jengo la ofisi mpya ya TAKUKURU Mkoa wa Mbeya.



Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru nchini, Dkt. Edward Hoseah pili kushoto  na mkuu wa mkoa wa Mbeya Abas Kandoro kushoto katika picha ya pamoja na viongozi Dini katika sherehe za uzinduzi wa jengo la ofisi mpya ya TAKUKURU Mkoa wa Mbeya.




Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru nchini, Dkt. Edward Hoseah akipokea zawadi kutoka kwa wafanyakazi wa TAKUKURU (Cofee Table) katika sherehe za uzinduzi wa jengo la ofisi mpya ya TAKUKURU Mkoa wa Mbeya
Afisa Elimu  kwa Umma TAKUKURU Mkoa wa Mbeya Ndugu Sala Chodota akitoa ufafanuzi kwa vilabu vya wanafunzi walio hudhuria sherehe hizo za uzinduzi wa jengo jipya za ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Mbeya .

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.