MTANGAZAJI

MAJINA YA MAWAZIRI WALIOPOTEZA MAJIMBO MPAKA SASA KATIKA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2015 NCHINI TANZANIA

 Wakati Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (NEC) ikiendelea kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa madiwani,wabunge na Rais nchini humo kwa mwaka 2015 ,tayali waliokuwa Mawaziri watano wa serikali ya awamu ya nne inayomaliza muda wake wamepoteza majimbo kwenye uchaguzi huo.

Mawaziri hao wanaungana na wabunge wengine  wa lililokuwa Bunge la Kumi walioshindwa kutetea majimbo yao,wakiwemo kambi ya upinzani ambao wameangushwa na wagombea wa chama tawala ambapo pia wamo mawaziri wa zamani wawili Cyril Chami na Omary Nundu.

Mawaziri waliopoteza majimbo ni Steven Wasira(Alikuwa Waziri wa Kilimo na Chakula,Christopher Chiza(Alikuwa Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji),Aggrey Mwanri (Alikuwa Naibu Waziri wa Tamisemi),Dr Steven Kebwe(Alikuwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii) na Anne Kilango(Alikuwa Naibu Waziri wa Elimu).

Uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu ukihusisha majimbo 264 kwa mujibu wa NEC ambapo waliojiandikisha kupiga kura ni 22,750,789 nchini humo huku idadi ya wanawake ikiwa ni 11,950,200,wanaume 10,800,589 na vituo vya kupigia kura vikiwa ni 65,105.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.