MTANGAZAJI

DAR ES SALAA:SERIKALI YA TANZANIA YAPOKEA MAJINA MAPYA YA MAHUJAJI WALIOPOTEZA MAISHA NA YA WENGINE AMBAO HAWAJAONEKANA


 3742683574_8989830a2b

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania kwa masikitiko makubwa imepokea majina mengine mawili ya Mahujaji kutoka Tanzania waliofariki dunia kufuatia tukio la mkanyagano wa Mahujaji lililotokea eneo la Mina, Makkah tarehe 24 Septemba, 2015 na kupelekea vifo vya Watanzania kufuatia tukio hilo kufikia watu saba (7) hadi sasa.

Majina ya Mahujaji hao ni Bw. Athumani Mateso Chaulana na Bw. Ahmed Said Bawazir ambao kupitia picha zao wametambulika kuwa wamefariki dunia.

Aidha, Wizara imepokea majina mapya 19 ya Mahujaji kutoka Tanzania ambao bado hawajaonekana. Itakumbukuwa kuwa tarehe 29 Septemba, 2015 Wizara ilitoa taarifa za kupatikana kwa majina 18 ya Mahujaji wa Tanzania ambao ni kati ya 50 ambao bado hawajaonekana. Kupatikana kwa majina hayo kunafanya idadi ya Mahujaji waliopotea na majina yao kutambulika kufikia 37.

Orodha ya majina mapya 19 ya Mahujaji wa Tanzania ambao mpaka sasa bado hawajaonekana ni kama ifuatavyo:-
1. Juma Bajuka
2. Masoud Juma
3. Issa Amir Faki
4. Juma Jecha Dabu
5. Nassor Mohammed Hemed
6. Mohamed Awadh Namongo
7. Juma Bakula
8. Said Habib
9. Hamis Juma Shamte
10. Khadija Hamad
11. Rahma Salim
12. Hadija Abdallah Sefu
13. Farida Khamis
14. Laila Manunga
15. Bi. Hawa Amrani Khamis
16. Saida Awadhi
17. Maimuna Seleman Ruwaly
18. Jalia Kassim Mashule
19. Nuru Omar Karama

Mbali na taarifa za kupatikana kwa majina hayo, Wizara imepokea taarifa ya kuonekana Mahujaji saba wakiwa hai. Mahujaji hao ni:-
1. Ali Abdulrahman (Abidina)
2. Abdallah Hassan Pande
3. Suleiman Ali Kidogoli
4. Mohammed Salum
5. Mwadini Hassan
6. Habiba Ramadhan Ali (Maulana)
7. Ramadhan Muhsin


Ubalozi kwa kushirikiana na Tanzania Hajj Missionna Vikundi vya Mahujaji unaendelea na juhudi za kuwatambua Mahujaji wengine wa Tanzania ambao hawajaonekana kwa kutembelea katika hospitali zilizohifadhi maiti na kulaza majeruhi wa ajali hiyo ikiwa ni pamoja na kuhakiki picha za mahujaji waliofariki ili kubaini Mahujaji kutoka Tanzania.

Wizara inapenda kufafanua kuwa, orodha inayotolewa si kamili kwa maana kwamba inaweza kuongezeka kwa vile baadhi ya majina ya Mahujaji yaliwayowasilishwa Ubalozini na ndugu wa mahujaji waliopotea hayamo katika orodha hii. 

Pia Ubalozi unaendelea kuwasiliana na vikundi vilivyopeleka Mahujaji ili kuweza kupata taarifa kamili na sahihi ya jumla ya Mahujaji wote ambao hawaonekani.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Dar es Salaam
30 Septemba, 2015

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.