RAIS KIKWETE AAGA UMOJA WA MATAIFA (UN)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete jumanne Septemba 29,2015 amelihutubia kwa mara ya mwisho Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mtaifa akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hotuba ya Mhe. Rais na ambayo iligusia mambo mengi ya kisiasa, kiuchumi, na maendeleo akitumia pia fursa hiyo kuwaanga viongozi wenzie na kuwashukuru kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi cha miaka kumi ya uongozi wake, iliwasisimua wajumbe wa mkutano huo kiasi cha kukatishwa mara kwa mara kwa makofi.
Zifuatazo ni baadhi ya picha zinazomwonyesha Mhe. Rais katika Matukio mbalimbali Moja wapo Zikiwa ni hafla ambayo Rais wa Marekani, Mhe Barack Obama aliiandaa kwaajili wa Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali waliohudhuria Mkutano wa 70 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Picha kwa hisani ya Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mhe.Barack Obama na Mkewe Michelle Obama wakati wa hafla ilioandaliwa na Rais wa Marekani kwaajii ya Viongozi wa Wakuu Nchi na Serikali wanaohudhuria Mkutano wa 70 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Mhe. Rais Kikwete akiwa na Mhe. Sophia Simba, Katibu Mkuu Balozi Liberata Mulamula na mwanamitindo Flaviana Matata muda mfupi mara baada ya kulihutubia Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa
Mwakilishi wa Kudumu wa Antigua na Bermuda Balozi Walton Alfonso Webson ambaye ni mlemavu wa kutoona akimwongoza Mhe. Rais Kikwete kwenda kuonana na Waziri Mkuu wake, Mhe. Gaston Alphoso Browne aliyekuwa na mazungumzo wa Mhe.Rais mara baada ya Mhe. Rais kulihutubia Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa.
Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Waziri Mkuu wa Antigua na Barbuda Mhe. Gaston Alphonso Browne, wengine katika mazungumzo hayo ni Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa kudumu wa Antigua na Barbuda, Balozi Walton Webson mwenye miwani myeusi na Mkurungezi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Celestin Mushy
Chanzo:Ikulu blog
Post a Comment