KIGOMA:WATU WASIOFAHAMIKA WATEKETEZA NYUMBA 8 KWA SIKU MBILI
Nyumba nane katika kijiji cha Kazilamihunda kata ya Kasanda
wilayani Kakonko mkoani Kigoma zimeteketezwa kwa moto na watu wasiofahamika
katika kipindi cha siku mbili mfululizo.
Mtendaji wa kijiji hicho Bw.Heziloni Mayunga amesema matukio hayo
yametokea usiku wa kuamkia jumatatu na kuamkia jumanne na kusababisha baadhi ya
wananchi kukimbia makazi yao na kulala porini wakihofia maisha yao.
Bw.Mayunga amesema kuwa usiku wa kuamkia jana nyumba nne
ziliteketezwa kwa moto na kusababisha hasara kubwa kwa wakazi hao ikiwemo
kuungua kwa mazao na mavazi.
Mmoja wa wahanga wa tukio hilo Bw.Rauliani Wilbadi amesema
kuwa kwa sasa wanapata wakati mgumu ambapo hulazimika kulala nje, hali ambayo
inahatarisha usalama wao.
Post a Comment