MTANGAZAJI

WAIMBAJI WA LIGHTBEARERS WAELEKEA JIJINI MWANZA KWA UZINDUZI WA VICTORY SINGERS

Waimbaji wa LightBearers toka Studio za JCB jijini Dar es salaam wamesafiri kuelekea jijini Mwanza kwenye uzinduzi wa santuri mwonekano mpya ya waimbaji wa Victory Singers wa jijini humo utakaofanyika jumapili Julai 12 mwaka huu.

Uzinduzi huo ambao utawashuhudia waimbaji wa Victory Singers ambao wamewasili jijini Mwanza jana baada ya kutoka nchini Kenya kwenye uzinduzi wa kituo cha radio utafanyika kwenye ukumbi wa Vijana ulioko Mlango mmoja ama Langolango huku ukiwahusisha pia waimbaji wa Sauti ya Jangwani toka Shinyanga, Zabron Singers toka Kahama na wengine wa jijini Mwanza.

Kiongozi wa LightBearers Waziri Barnabas (Chifu) amesema wanaelekea jijini Mwanza kushiriki tamasha hilo ili kuwaunga mkono Victory Singers pia kutokana na hitaji la muda mrefu la wapenzi wa nyimbo za injili wa jijini Mwanza kuwashuhudia waimbaji wengine toka jijini humo ambao wamekuwa wakifanya matamasha nje ya MwanzaNo comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.