AMBASSADORS OF CHRIST WAREKODI SANTURI MWONEKANO YA 12
Waimbaji
wa Ambassadors Of Christ toka Kigali, Rwanda, juni 5 mwaka huu
walifanya tamasha la aina yake katika Chuo Kikuu cha Afrika ya Kati cha
Waadventista katika eneo la Gishushu huko Rwanda kwa lengo la kurekodi
video ya santuri mwonekano waliyoipa jina la FATA UMWANA WESE NKU WAWE
ambayo imejikita katika kueleza madhara ya madawa ya kulevya kwa vijana
katika jamii.
.Toleo
hilo lenye nyimbo za Kinyarwanda ni la 12 toka waimbaji hao waanze
kuimba mwaka 1995, kwa lengo la kutangaza injili na kuwaunganisha
wanyarwanda baada ya mauaji ya kimbali ya mwaka 1994.
Waimbaji
wengine walioshiriki kwenye tamasha la kurekodi video ya santuri hiyo
ni Shalom, Friends of Jesus, Paradise Melody, Epedusalut, Patmos,
Maranatha Men, Maranatha Family na Orion Singers.
Post a Comment