DAR ES SALAAM:WAJUMBE WA TUZO YA JAMII WATEMBELEA UKUMBI KUTAKAKOFANYIKA UTOAJI WA TUZO HIYO MWAKA HUU
Ndani ya Ukumbi kutakakofanyika hafla ya utoaji wa Tuzo ya Jamii |
Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya Tuzo ya Jamii ndani ya ukumbi. |
Katibu wa Tuzo ya Jamii Amani Theophilas Mwaipaja akisisitiza jambo |
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tuzo ya Jamii DJ Malegesi akiwa na Mhandisi Sylvester Mayunga (Mjumbe) |
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tuzo ya Jamii itayotolewa Aprili 13 mwaka huu wametembelea katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Center (JNICC) ambako kutafanyika hafla ya utoaji wa Tuzo hiyo.
Tuzo hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya Tanzania Awards International Limited itakuwa katika kipengele cha Tuzo
ya Jamii ya heshima itakayotolewa kwa Rais wa awamu ya kwanza wa Tanzania Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa kwanza wa Afrika Kusini Hayati Nelson
Mandela.
Pamoja na Tuzo hiyo ya
heshima pia itatolewa Tuzo ya Haki za binadamu ambapo mshindi atatangazwa siku
hiyo, Tuzo kwa mwanasiasa kijana na
mwanasiasa mtu mzima mwenye mafanikio
katika siasa za Tanzania.
Washindi wa siasa watapatikana baada ya
kupigiwa kura kupitia huduma ya simu ya mkononi ya PUSH ambapo vigezo
vya kutazama unapopiga kura kuwa ni pamoja na
uvumilivu katika siasa ,uwezo wa kuibua na kutetea hoja ,ushiriki wake
katika kutetea maslahi ya Taifa,ushiriki wake katika huduma za Jamii na Nidhamu
katika shughuli zasiasa.
Hii itakuwa ni mara ya Kwanza nchini Tanzania kwa Kampuni ya Tanzania Awards Internation Limited kutoa Tuzo ya Heshima kwa viongozi hao huku mgeni rasmi katika hafla hiyo akitarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.
Post a Comment