ARUSHA:CHUO KIKUU CHA ARUSHA CHAELEZA ALIYOYAFANYA MCHUNGAJI NICANOR KIKIWA WAKATI AKIWA MWANAFUNZI CHUONI HAPO
Marehemu Mchungaji Nikanor Kikiwa (Pichani) aliyefikwa na mauti Februari 17,2015 katika hospitari ya Dar Group amezikwa leo huko Morogoro.
Nikanor aliyezaliwa mwaka 1980 alijiunga na Chuo Kikuu cha Arusha Januari 8,2004 na kuhitimu masomo yake ya
shahada ya kwanza ya Thiolojia Julai
2,2007.
Akiwa anasoma katika Chuo kikuu cha Arusha marehemu Nikanor Kikiwa
alijituma sana kwenye masomo na kuonyesha juhudi kubwa ya mambo ya kiroho na ushirikiano mzuri na
wanafunzi wenzake, waalimu na jamii nzima kwa ujumla.
1.Marehemu Mch Nikanor Kikiwa aliwahi kuwa mmoja
wa viongozi wa chama cha wachungaji Chuo Kikuu cha Arusha yaani University of Arusha Ministeral Association na kupitia
uongozi wake,wachungaji waliokuwa wanasoma kipindi hicho walisaidia wanachuo
wengine kuwa na maadili mema chuoni hapo.
2.Alikuwa mwimbaji katika vikundi vya Harvest Brothers,Pilgrims na Early Melodies vilivyoboresha
program mbalimbali za kiroho na
kukitangaza Chuo.
3.Alikuwa mtanashati jambo ambalo
lilisababisha wanafunzi wenzake kuguswa
na kubadilika nakuwa watanashati.
4.Aliuanza uchungaji wake hata kabla
hajamaliza masomo kwani akiwa chuokikuu cha Arusha alitumia muda wa jioni
kushauri wanafunzi wenzake na kutembelea washiriki na wasio washiriki kwalengo
la uinjilisti(Ucheshi ulimuwezesha kuwa na marafiki wengi).
5.Alijituma sana katika programu za vijana na
alifanya kwa vitendo kile alichokuwa anakifanya Darasani jambo ambalo
lilisaidia Chuo Kikuu cha Arusha kuwa na
timu ya Masterguide nzuri kipindi chake akiwa chuoni.
6.Alikuwa na Ujasiri muwazi hakuogopa kuitaja
dhambi kwa jina alipoona wanafuzi wenzake wanakosea aliwaendea nakuwaambia hapo
umekosea hili halikuishia kwa wanafunzi wenzake tuu hata kwa wakufunzi Alikuwa
mtu wa Kiroho.
Chuo Kimempoteza ALUMNI wake ambaye alikuwa
mstari wa mbele kutoa mawazo ya namna ya kuboresha Chuo kikuu cha Arusha .
Imetolewa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma wa Chuo Kikuu cha Arusha
Post a Comment