DAR ES SALAAM:MAANDALIZI YA MISSION EXTRAVAGANZA YAENDELEA KUPAMBA MOTO
Mwenyekiti wa Unioni ya Kusini mwa Tanzania ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Mch Magulilo Mwakalonge (Mwenyesuti) akiteta jambo na baadhi ya wajumbe. |
Mkurugenzi wa Morning star Radio Mch Lusekelo Mwakalindile aliyevaa suti wakipongezana na aliyewahi kuwa Mhazini wa iliyokuwa Taasis ya Vyombo Vya Habari vya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Tanzania (TAMC) Coheleth Manumbu baada ya kumaliza kikao cha Maandalizi ya Mkutano wa Sherehe za Utume uliofanyika katika kanisa la sabato Ilala jijini Dsm (Picha zote na Jackson Sekiete) |
Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Maandalizi ya mkutano wa Sherehe za Utume (Mission Extravaganza) wa kanisa la Waadventista Wa Wasabato Mchungaji Rabson Nkoko amesema maandalizi ya mkutano huo unatarajiwa kufanyika jijini Dar es salaam kuanzia Februari 1 hadi 7,2015 yamekamilika.
Jana Januari 18 katika kanisa la Waadventista Wa Sabato Ilala jiji Dar es salaam,wajumbe toka katika konferensi mbili za Mashariki mwa Tanzania ikiwemo ile ya kati na ya kusini wakiwa na Viongozi wa Union ya Kusini mwa Tanzania walikutana ili kutathimi maadalizi ya kufanikisha mkutano huo ambao utahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kanisa hilo akiwepo mkuu wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Mch Tedy Wilson ambaye itakuwa mara yake ya kwanza kufika Tanzania toka apewe wadhifa huo miaka minne iliyopita.
Post a Comment