UMEZIONA ALAMA ZA BARABARANI ZINAZOENDELEA KUWEKWA KATIKA BARABARA MPYA JIJINI DAR ES SALAAM?
Alama ya juu ikilazimisha kusimama ya chini inaeleza kuna magari yanayokwenda kushoto |
Hapa kuna kituo cha waenda kwa miguu na kuna tuta ama kuna kituo cha waenda kwa miguu ambacho kiko katika tuta |
Alama ya kituo cha mabasi cha Kagera |
Alama ya nenda kushoto |
Wakati hatua za mwisho mwisho za kukamilisha ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo kasi jijini Dar es salaam,baadhi ya baraba hizo zimeshaanza kuwekewa alama za barabarani ambazo hazikuwepo kabla ya ujenzi huo.
Alama za barabarani hapa nchini ziko katika makundi yafuatayo:
1.Alama za Amri zinazotoa kipaumbele
2.Alama za Amri zinazolazimisha
3.Alama za Maonyo
4.Alama za Taarifa
Ukipita katika barabara kuu ya Ubungo kwa maana eneo kutoka fire hadi kituo cha mabasi cha ubungo utaziona alama hizi zikiwa zimewekwa kwa sasa na zingine zikiwa zinaandaliwa kuwekwa.
Post a Comment