DAR ES SALAAM:KONGAMANO LA TAIFA LA WATOTO WANAOISHI NA VVU/UKIMWI KUFANYIKA KESHO
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana
na Shirika la huduma za watoto la Elizabeth Glaser Pediatric Foundation (EGPAF),UNICEF
na wabia wengine wa huduma za Virusi vya UKIMWI (VVU) pamoja na Chama cha Madaktari
wa watoto Tanzania (PAT) imeandaa kongamano la nne la Taifa la watoto wanaoishi
na VVU/ UKIMWI.
Akizungumza na waandishi wa habari jiji Dar es
salaam mapema leo, Mratibu wa huduma za UKIMWI kwa watoto Dr Aneth Rwebembera amesema kuwa kongamano hilo linatarajia
kufanyika tarehe 19 na 20 Nov 2014 katika kituo cha mikutano ya kimataifa cha Mwl Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Ameongeza kuwa kauli mbiu ya kongamano hilo ‘’Kuongeza Kasi’’ Ikiwa ni kuimarisha upatikanaji wa huduma,vipimo, matunzo na tiba ya VVU
ili kuboresha maisha ya mtoto.
Kongamano hilo linatarajiwa kuhudhuriwa na wajumbe
mbalimbali wakiwemo washiriki wa kitaifa na kimataifa wanaojihusisha na udhibiti wa VVU kwa
watoto,wawakilishi kutoka Wizara za serikali, wabia wa maendeleo na mashirika
mengine,huku lengo ni kuongeza uelewa wa taifa wa mikakati mipya ya utoaji
huduma ya kudhibiti VVU na kuuelimisha umma kuhusu hali ya sasa kuhusianan na
huduma za VVU/UKIMWI kwa watoto.
Post a Comment