DAR ES SALAAM:KAMATI KUU YA UTENDAJI YA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO KUSINI MWA TANZANIA YAFANYA KIKAO CHAKE
Kamati kuu ya utendaji kazi ya kanisa la Waadventista Wasabato Union ya Kaskazini mwa Tanzania imezindua kikao chake
cha pili cha mwisho wa mwaka mapema hii leo katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato mwenge
jijini Dar es salaam.
Katibu wa Mkuu wa Union
ya Kusini mwa Tanzania Mch James Machage
amesema kuwa lengo kuu la kikao hicho ni kutoa ripoti za utendaji kazi wa idara
zote zilizopo ndani ya union ya kusin mwa Tanzania.
Mchungaji James Machage ameongeza kuwa kikao hicho
pia kinalenga mipango na mikakati ya kazi ya injili kwa mwaka 2015.
Aidha Mchungaji Machage ametoa wito kwa wakazi
wa jiji la Dar es salaam kuhudhuria katika kanisa la Waadventista Wa Sabato Mwenge siku ya kesho saa mbili asubuhi kwa ajili kusikiliza taarifa za utendaji
kazi wa idara mbalimba zilizopo ndani ya kanisa.
Kikao hicho kilichozinduliwa hii leo
kinatarajia kuendelea mapema kesho asubuhi kikihudhuriwa na viongozi wote wa Union ya Kusini mwa Tanzania viongozi wote wa majimbo ya mashariki mwa Tanzania na
jimbo la nyanda za juu za kusini pamoja na viongozi wa idara mbalimbali pia kikihudhuriwa na viongozi toka Division ya Afrika Mashariki na Kati.
Post a Comment