MANYARA:JAMII YATAKIWA KUHESHIMU NDOA

Mkurugenzi wa Idara ya huduma za wanawake,watoto na shule ya Sabato Konferensi ya Nyanza Kusini ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Bi
Esther Malyeta (Pichani) ameitaka jamii
kuziheshimu ndoa ili kujenga kizazi bora cha leo na baadae .
Akihutubia mamia ya wakazi wa mji wa Haydom Mkoani Manyara
jana jioni Bi Malyeta ambaye aliwahi kuwa mkuu wa wilaya ya Hanang na
Sengerema amesema kuwa familia nyingi
zimesambaratika kutokana na kukosekana kwa
upendo na huruma ndani ya ndoa.
Bi Malyeta amesema kuwa
kama ndoa hazitaheshimiwa watoto wa waishio katika mazingira magumu
hawatapungua kamwe,kwa kuwa watoto wengi walioko waishio katika mazingira
magumu sio kwamba hawana wazazi bali wazazi wao wamefarakana hivyo imewalazimu
kutawanyika kuhitaji msaada wa kuishi.
Ameeleza kuwa inashangaza kuona mume anampiga mke wake hali
kadhalika mke kumpiga mume wake kwani Biblia inaeleza kuwa mume na mke ni mwili
mmoja sasa yawezekanaje mtu kujipiga mwenyewe.
Nao wakazi wa Mji wa
Haydom wamesema kuwa uwepo wa mkutano wa injili
unaoendeshwa na Idara ya wanawake wa Unioni konferensi ya kaskazini mwa
Tanzania katika viwanja vya CCM mjini Haydom utaibadilisha jamii kumwelekea
mungu kupitia mafundisho mbalimbali yahusuyo wokovu na maadili mema ambao wa kwanza
kuwepo mahali kwenye eneo hilo tangu kanisa la waadventista wasabato
lilipojengwa na kusimikwa mjini humo.
Mkutano huo ulianza siku ya Jumapili kwa ufunguzi rasmi
uliofanywa na diwani wa kata ya Haydom mheshimiwa Nathanieli Nasasu utahitimishwa Novemba
2,2014.
Post a Comment