ARUSHA:MWANAMKE ATUHUMIWA KUMBAKA NA KUMKATA ULIMI KIJANA WA KIUME
Kijana mmoja mkazi wa Kimandolu jijini Arusha, Paulo Simon
mwenye umri wa miaka 18 amelazwa katika hospitali ya mkoa Mount Meru baada ya kubakwa
na kisha kukatwa ulimi na mwanamke mmoja aliyekuwa akimtaka kimapenzi .
Tukio hilo la kusikitisha limetokea jana majira ya saa 6.30
usiku katika eneo la Tindigani,kimandolu ,wakati mwanamke huyo aliyetambulika
kwa jina moja la mama Abuu alipofika katika bar hiyo kama mteja na baadaye
alimlazimisha mhudumu wa bar hiyo ambaye ni majeruhi kufanya mapenzi bila
ridhaa yake.
Simoni ambaye ni mfanyakazi katika bar hiyo, inayomilikiwa na
mwenyekiti wa mtaa ,Joel Mbasha alisema mnamo majira ya usiku alikuja mwanamke huyo na kuagiza
kinywaji huku yeye akimhudumia kabla hajamgeuzia kibao .
Alieleza kuwa ilipotimu majira ya saa 6.30 wateja waliisha
katika bar hiyo na kuamua kufunga bar ,hata hivyo mwanamke huyo ndiye aliyebaki
pekee akinywa pombe taratibu katika eneo hilo ndipo alipomlazimisha kufanya
kitendo hicho ambapo alimziba mdomo kwa kutumia kinywa chake na baadae
alifanikiwa kumng’ata ulimi na kuutema chini.
Majeruhi huyo kwa sasa hali yake bado mbaya kwani hawezi
kuongeza na muda mwingi anatokwa na damu nyingi hatua ambayo imewalazimu
wahudumu katika hospitali hiyo kumwekea ndoo ya kutemea damu.
Jeshi la polisi mkoani Arusha limethibitisha tukio hilo na
kwamba mtuhumiwa anashikiliwa na upelelezi utakapokamilika atafikishwa
mahakamani.
Post a Comment